Monday, July 3, 2017

FIFA KOMBE LA MABARA: GERMANY WABEBA KOMBE, CHILE CHINI YAKUBALI KICHAPO. PORTUGAL WASHIKA NAFASI YA 3

Germany, wakiwa na Kikosi tofauti na kile kilichotwaa Kombe la Dunia huko Brazil Mwaka 2014, Jana wametwaa Ubingwa wa Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara walipowafuga Mabingwa wa Marekani ya Kusini Chile 1-0 Uwanjani Saint Petersburg Stadium Mjini Saint Petersburg Nchini Russia.
Bao la ushindi la Germany lilifungwa Dakika ya 20 na Lars Stindl kufuatia kosa la Marcelo Diaz.

Hii ni mara ya kwanza kwa Germany kutwaa Kombe hili.
Mapema Jana, katika Mechi ya kusaka Mshindi wa 3, Portugal ilitoka nyuma kwa Bao Bao 1-0 na kuifunga Mexico 2-1 katika Dakika za Nyongeza 30.
Mexico walitangulia kufunga kwa Bao la kujifunga wenyewe la Luis Neto na Pepe kusawazisha na Gemu kwenda Dakika za Nyongeza 30.
Adrien Sival aliipa Bao Portugal la Penati katika muda huo wa Nyongeza.

Chile 0-1 Germany: World champs win Confed Cup final in St. Petersburg (as it happened)