Wednesday, July 19, 2017

INTERNATIONAL CHAMPIONS CUP: ARSENAL YAIFUNGA BAYERN KWA PENATI 3-2 LEO

Bao la kusawazisha la Dakika ya 94 la Alex Iwobi liliwapa Sare ya 1-1 Arsenal walipocheza na Bayern Munich huko Shanghai na kisha kupata ushindi wa 3-2 kwenye Mikwaju ya Penati Tano Tano kwenye ya kugombea International Champions Cup.
Bayern ndio waliopata Bao la kuongoza kwa Penati ya Dakika ya 9 iliyofungwa na Robert Lewandowski aliemchambua Kipa Petr Cech.
Penati hiyo ilitolewa kufuatia Ainsley Maitland-Niles kumsukuma Juan Bernat.

Bao hilo lilidumu hadi Dakika 90 kugonga na kwenye Dakika ya 4 ya muda wa Majeruhi Iwobi akaisawazishia Arsenal kwa Kichwa alipounga Krosi ya Aaron Ramsey.
Hadi mwisho Arsenal 1 Bayern 1.
Ndipo ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano na Bayern kukosa 3 zilizopigwa na David Alaba, Sanches and Bernat wakati Ramsey, Nacho Monreal na Iwobi wakiifungia Arsenal.

Alexandre Lacazette played the first 45 minutes for Arsene Wenger's sideVIKOSI VILIVYOANZA: Arsenal XI: Petr Cech; Krystian Bielik, Per Mertesacker, Nacho Monreal, Ainsley Maitland-Niles; Francis Coquelin, Granit Xhaka, Sead Kolasinac, Mesut Ozil; Danny Welbeck, Alexandre Lacazette.
Bayern Munich XI: Tom Starke, Rafinha, Juan Bernat, Mats Hummels, David Alaba; Corentin Tolisso, Franck Ribéry, Javi Martínez, Thomas

Arsenal – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:
13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney [2-0]
15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney [3-1]
19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup (1-1, Penati 3-2)
22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)
29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)
30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)
6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)