Wednesday, July 12, 2017

JAMES RODRIGUEZ ATIMKIA KWA MKOPO BAYERN KWA MIAKA 2.

https://img.fcbayern.com/image/fetch/f_auto,h_768,q_auto:good,w_1366/https://fcbayern.com/binaries/content/gallery/fc-bayern/homepage/saison-17-18/galerien/james-erster-tag/10-james_get_120717.jpg/10-james_get_120717.jpg/fcbhippo%253Axtralargesixteentonine%3Fv%3D1499859365879James Rodriguez amejiunga na Bayern Munich kutoka Real Madrid kwa Mkopo wa Miaka Miwili.
Rodriguez, Mchezaji wa Kimataifa wa Colombia, amekuwa hana namba ya kudumu kwenye Timu ya Real iliyo chini ya Kocha Zinedine Zidane na Mwezi uliopita hakuwemo kabisa katika Kikosi cha Real kilichoichapa Juventus 4-1 katika Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI iliyochezwa Mjini Cardiff huko Wales.
Staa huyu mwenye Miaka 25 amekuwa akihusishwa na kujiunga na Manchester United huku pia Wakala wake akimtangaza kwa Klabu za Chelsea, Liverpool, Paris Saint-Germain, Inter Milan na Juventus.

Lakini Rodriguez, aliejiunga na Real Mwaka 2014 kutoka AS Monaco kwa Dau la Pauni Milioni 71, ameamua kucheza kwa Mabingwa wa Germany Bayern Munich akijumuika tena Kocha Carlo Ancelotti ambae ndie alimpeleka Real alipokuwa Kocha Mkuu wa Vigogo hao wa Spain.
Rodriguez aliichezea Real Mechi 111 na kufunga Bao 36.
Staa huyo atajiunga na Bayern Jumapili ijayo tayari kwa Tripu ya Siku 12 huko China na Singapore.