Thursday, July 13, 2017

LACAZETTE APIGA BAO MECHI YAKE YA KWANZA HUKO SYDNEY, ARSENAL 2-0 MBELE YA MASHABIKI 80,000

Alexandre Lacazette got his Arsenal career off to a perfect start with a goal on his first appearance for the clubARSENAL imeanza Ziara yake ya Matayarisho kwa ajili ya Msimu Mpya wa 2017/18 kwa kushinda Mechi yao ya kwanza huko Sydney, Australia walipoichapa Sydney FC 2-0 mapema hii Leo Mchana mbele ya Mashabiki 80,432 ndani ya ANZ Stadium.
Granit Xhaka runs over as Eddie Nketiah and Alex Iwobi celebrate with Lacazette after opening his accountKwa Mashabiki wa Arsenal, furaha kubwa ni kumuona Mchezaji wao Mpya, Alexander Lacazette, akitokea Benchi na kuonyesha cheche zake kwa kupiga Bao la Pili Dakika ya 83.
Bao la Kwanza la Arsenal lilifungwa Dakika ya 4 tu na Beki Per Mertesacker kufuatia kizaazaa cha Kona.

Per Mertesacker scored the opening goal of the game as he hooked the ball home to get his side off and running in SydneyMechi ya Pili ya Arsenal ni huko huko Australia ndani ya ANZ Stadium Jijini Sydney dhidi ya Western Sydney Wanderers na kisha kupaa kwenda China kuzivaa Bayern Munich na Chelsea.
It may only have been a friendly, but Mertesacker and the Arsenal players were delighted by their opening goal
Arsenal - Mechi kuelekea Msimu Mpya:
13 Julai v Sydney FC, ANZ Stadium, Sydney
15 Julai v Western Sydney Wanderers, ANZ Stadium, Sydney
19 Julai v Bayern Munich (Shanghai Stadium) International Champions Cup
22 Julai v Chelsea (Bird’s Nest Stadium, Beijing)
29 Julai v Benfica, Emirates Stadium (Emirates Cup)
30 Julai v Sevilla, Emirates Stadium (Emirates Cup)
6 Agosti v Chelsea, Wembley Stadium (Community Shield)