Sunday, July 23, 2017

LEO JUMAPILI USIKU SAA 6, MAN UNITED KUIVAA REAL MADRID HUKO USA

JUMAPILI Usiku, Sasa 6 kwa Saa za Bongo, Manchester United wataingia Levi’s Stadium, Santa Clara, California, USA, kupambana na Mabingwa wa Spain na Ulaya Real Madrid katika Mechi ya International Champions Cup.
Mechi hi ya Kirafiki ni Mechi ya 4 kwa Man United katika Ziara yao huko USA ambako walizifunga LA Galaxy, Real Salt Lake na Mahasimu wao Manchester City.
Kwenye Ziara hiyo, Wachezaji Wapya Victor Lindelof na Romelu Lukaku wameonyesha uwezo mkubwa huku Lukaku akifunga Bao kadhaa.
Kwenye Mechi hii na Real, Meneja Jose Mourinho amedokeza kuwa watatumia Mfumo wa Beki 4 huku Lindelof akicheza Sentahafu.
Mchezaji pekee mwenye hatihati kucheza Mechi hii ni Juan Mata ambae aliumia Enka kwenye Mechi na Real Salt Lake City.

Kwa upande wa Real, chini ya Kocha Zidane Zidane, Mechi hii ni ya kwanza kwao katika matayarisho ya Msimu Mpya na watamkosa Staa wao mkubwa Cristiano Ronaldo ambae amepewa likizo ndefu baada ya kushiriki Mashindani ya FIFA ya Kombe la Mabara akiiwakilisha Nchi yake Portugal huko Russia.

Mbali ya Mechi hii ya Kirafiki, Timu hizi zitapambana tena Agosti 8 huko nchini Macedonia kugombea UEFA SUPER CUP Kombe ambalo hushindaniwa na Bingwa wa UEFA CHAMPIONS LIGI na yule alietwaa UEFA EUROPA LIGI.

Real walitwaa UEFA CHAMPIONS LIGI kwa kuitwanga Juventus 4-1 na Man United kubeba UEFA EUROPA LIGI kwa kuifunga Ajax Amsterdam 2-0.