Wednesday, July 19, 2017

MAN UNITED - ZIARA: REAL SALT LAKE 1 vs 2 MAN UNITED, LUKAKU AFUNGUA BAO LA USHINDI

WAKICHEZA Mechi yao ya pili ya Ziara yao ya huko USA, Manchester United walitoka nyuma kwa Bao 1 na kuichapa Real Salt Lake 2-1 kwenye Mechi iliyochezwa ndani ya Rio Tinto Stadium, Utah.
Real ndio waliotangulia kwa Bao la Dakika ya 20 la Luis Silva aliepokea Pasi safi ya Jefferson Savarino na kumzidi akili Kipa Joel Pereira.
Man United waliweza kusawazisha Dakika ya 29 Mfungaji akiwa Henrik Mkhitaryan.
Katika Dakika ya 33, Real walibadili Wachezaji 11 kwenye Timu yao.
Kisha Mchezaji Mpya Romelu Lukaku, akianza Mechi yake ya kwanza kabisa, alipiga Bao la Pili na la ushindi katika Dakika ya 38 baada pande zuri toka kwa Mkhitaryan.
Nae Jose Mourinho alibadili Wachezaji 11 wa Man United wakati wa Haftaimu na kaikati ya Kipindi cha Pili, Antonio Valencia alipewa Kadi Nyekundu kwa Rafu mbaya aliyomchezea Sebastian Saucedo ambae muda mfupi kabla alimuumiza Juan Mata na kulazimisha Mcezaji huyo kutolewa nje na kubadilishwa na Chipukizi Mitchell.
VIKOSI:
Real Salt Lake - Kipindi cha Kwanza: Rimando, Beltran, Glad, Horst, Phillips, Beckerman, Stephen, Savarino, Rusnak. Plata, Silva.
Real Salt Lake - Baada Dakika 33: Fernandez, Wingert, Silva, Maund, Acosta, Brody, Mulholland, Besler, Saucedo, Hernandez, Lennon.
Man United - Kipindi cha Kwanza: J Pereira, Fosu-Mensah, Lindelof, Jones, Blind, Carrick, Pogba, McTominay, Lingard, Mkhitaryan, Lukaku.
Man United - Kipindi cha Pili: Romero, Valencia, Bailly, Smalling, Darmian, Herrera, Fellaini, A Pereira, Mata (Mitchell 59), Martial (Tuanzebe 90), Rashford.


Manchester United – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:

15 Julai v LA Galaxy, Stubhub Centre, Los Angeles [5-2]
17 Julai v Real Salt Lake, Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah (2-1)
20 Julai v Manchester City, NRG Stadium, Houston, Texas (International Champions Cup)
23 Julai v Real Madrid, Levi’s Stadium, Santa Clara, California (International Champions Cup)
26 Julai v Barcelona, FedExField, Washington DC (International Champions Cup)
30 Julai v Valerenga, Ullevaal Stadium, Oslo
2 Agosti v Sampdoria, Aviva Stadium, Dublin
8 Agosti v Real Madrid, National Arena Filip II, FYR Macedonia (UEFA Super Cup)