Monday, July 10, 2017

MANCHESTER UNITED – MSIMU MPYA 2017/18: LEO MOURINHO NA WACHEZAJI 27 WAPAA ZIARANI USA

New signing Victor Lindelof relaxes on board the flight ahead of the pre-season tourMENEJA wa Manchester United Jose Mourinho ameteua Wachezaji 27 kwenda Los Angeles, United States of America kwa Ziara ya Mazoezi na Mechi za Kujipima nguvu kabla kuuanza Msimu Mpya wa 2017/18 Mwezi Agosti.
Miongoni mwa hao 27 ni Mchezaji Mpya Victor Lindelof na Chipukizi Scott McTominay na Demetri Mitchell.
Wakiwa huko USA, Man United watacheza Mechi 5.
Mechi ya kwanza ni Jumamosi ijayo dhidi ya LA Galaxy na Masaa 48 kuivaa Real Salt Lake.
Juan Mata and David De Gea smile for the camera on board Manchester United's flightKisha zitafuata Mechi dhidi ya Manchester City, hapo Julai 20 huko Houston, ikiwa Mechi ya kwanza na Mahasimu wao hao nje ya England, na kisha kucheza na Real Madrid Julai 23 huko Santa Clara na Barcelona hapo Julai 26 huko Washington DC.
Baada kuondoka USA, Man United watacheza Mechi 2 Nchini Norway na Ireland dhidi ya Valerenga hapo Julai 30 huko Oslo na Sampdoria ya Italy huko Dublin hapo Agosti 2.
Mbali ya Kikosi hicho cha Wachezaji 27, Mchezaji Mpya Romelu Lukaku anatarajiwa kujiunga nao baada ya kukamilika taratibu zote za Uhamisho wake kutoka Everton.

Ashley Young with Marcus Rashford (centre) and Jesse Lingard on the flight to Los AngelesMAN UNITED – KIKOSI KILICHOPAA LEO: 
De Gea, Romero, J Pereira, Valencia, Darmian, Fosu-Mensah, Bailly, Blind, Jones, Smalling, Lindelof, Tuanzebe, Rojo, Shaw, Mitchell, Young, Carrick, Fellaini, Herrera, McTominay, Pogba, Lingard, Mkhitaryan, Mata, A Pereira, Martial, Rashford.

Manchester United – Mechi za Matayarisho:
15 Julai v LA Galaxy, Stubhub Centre, Los Angeles
17 Julai v Real Salt Lake, Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah
20 Julai v Manchester City, NRG Stadium, Houston, Texas (International Champions Cup)
23 Julai v Real Madrid, Levi’s Stadium, Santa Clara, California (International Champions Cup)
26 Julai v Barcelona, FedExField, Washington DC (International Champions Cup)
30 Julai v Valerenga, Ullevaal Stadium, Oslo
2 Agosti v Sampdoria, Aviva Stadium, Dublin
8 Agosti v Real Madrid, National Arena Filip II, FYR Macedonia (UEFA Super Cup)