Monday, July 3, 2017

MORATA HUYOO MAN UNITED KWA KITITA CHA £64m

WAWAKILISHI wa Straika wa Spain Alvaro Morata wamekutana na Real Madrid Asubuhi hii kujadili hatima ya Straika huyo anaetaka kwenda Manchester United.
Manchester United wanataka kumsaini Morata ili ambadili Zlatan Ibrahimovic huku akiafiki Uhamisho huo.
Hii Leo, Wakala wa Morata, Juanma Lopez, na Baba Mzazi wa Mchezaji huyo, Alfonso Morata, walitua huko Santiago Bernabeu Jijini Madrid na kufanya Mazungumzo ya Dakika 50 na Real Madrid.

Man United na Real zimekuwa zikivutana kuhusu Dau la Uhamisho ambalo Real wanataka Zaidi Pauni Milioni 70 kwa Straika huyo wa Miaka 24 wakati Man United walishatoa Ofa ya Pauni Milioni 52.4.