Tuesday, July 4, 2017

MTOTO WA GEORGE WEAH TIMOTHY ASAINI PSG

Related imageImage result for Timothy Weah  TO PSGTimothy Weah sasa ameanza kufuata Nyayo za Babaye aliewahi kutwaa Ballon d'Or, George Weah, kwa kusaini Mkataba wa kucheza Soka la Kulipwa na Paris St-Germain ya France.
Kijana huyo mwenye Miaka 17 amesaini PSG ambayo Baba yake, Lejendari wa Liberia na Afrika, aliichezea kati ya Mwaka 1992 na 1995. Kinda huyo anadokezwa kuwa amerithi mikoba ya ufundi wa Baba yake.
Mwezi Septemba 2016, Timothy alipiga Hetitriki wakati akicheza Mechi yake ya kwanza kabisa walipoitwanga Ludogorets 8-1 kwenye Mashindano ya Vijana ya Ligi ya UEFA.
Timothy Weah, ambae alizaliwa New York, USA kabla kujiunga na Chuo cha Vijana wa PSG Julai 2014, amesema anasikia fahari kubwa kusaini kucheza Profeshenali na PSG.
George Weah, mwenye Miaka 50, amewahi kuwa Mchezaji Bora Afrika mara 3 na ni Mwafrika pekee kutwaa Tuzo ya Ballon d'Or Mwaka 1995 ambayo hutunukiwa Mchezaji Bora Duniani.

Wateah alijenga Jina lake akiwa na AS Monaco Mwaka 1988 na pia kupata mafanikio makubwa akiwa na Klabu za PSG na AC Milan.
Pia aliwahi kuzichezea Chelsea na Manchester City wakati Soka lake likielekea machweo.