Monday, July 10, 2017

RASMI..ROMELU LUKAKU ATUA OLD TRAFFORD, ASAINI MKATABA.

Romelu Lukaku has completed his Manchester United medical
KLABU KIGOGO ya Manchester United imethibitisha kuwa Straika Romelu Lukaku sasa ni Mchezaji wao rasmi baada ya kusaini Mkataba wa Miaka Mitano.
Man United imewalipa Everton Pauni Milioni 75 na inasemekana Dau hilo litapanda kwa nyongeza ya Pauni Milioni 15 kutegemea na kufikiwa kwa Vipengele kadhaa vinavyohusiana na mafanikio na Mechi atakazocheza.
Mabingwa wa England Chelsea walitaka sana kumrejesha kwao Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Belgium mwenye Miaka 24 lakini mwenyewe akaichagua Man United.
Chelsea walimsaini kutoka Anderlecht Agosti 2011 kwa Pauni Milioni 18.
Baadae Lukaku akakopeshwa kwa West Bromwich Albion na Everton kabla Julai 2014 Everton kuilipa Chelsea Pauni Milioni 20 na kumnunua moja kwa moja.

Akiongea mara baada ya Lukaku kusaini Mkataba, Meneja wa Man United Jose Mourinho ameeleza: “Romelu ni Mchechaji stahiki kwa Man United. Ana haiba kubwa na ni Mchezaji mubwa. Ni kawaida yeye kutaka kuendeleza Soka lake kwenye Klabu kubwa. Ni nyongeza safi sana kwa Kikosi chetu. Nangojea kwa hamu kufanya nae kazi tena.”

Romelu Lukaku kept his followers up to date with his medical this morning
Nae Lukaku, ambae Mkataba wake na Man United una Kipengele cha Nyongeza ya Mwaka Mmoja, ameeleza: “Pale Manchester United na Jose Mourinho walipokuja kugonga Mlangoni kwangu, nikajua ni nafasi pekee katika maisha yangu na sikuweza kuikataa. Nangoja kwa hamu kubwa kutinga Old Trafford mbele ya Mashabiki 75,000!”
Kwa sasa Lukaku yupo huko USA ambako atajiunga na Kikosi cha Man United kilichokwenda huko kwa ajili ya matayarisho ya Msimu Mpya.

LUKAKU – TAKWIMU:
-Msimu uliopita Lukaku, aliifungia Everton Bao 2 Mwezi Machi na kufikisha Bao 20 za Ligi kwa Msimu Mmoja na kuikamata Rekodi ya Gary Lineker aliyoiweka Msimu wa 1985/86 akiichezea Everton.

-Lukaku ni Mchezaji wa 4 kufunga Bao zaidi ya 80 katika EPL, LIGI KUU ENGLAND, kabla kutimiza Umri wa Miaka 24 wengine wakiwa ni Michael Owen, Robbie Fowler na Wayne Rooney.

-Katika Historia ya EPL, Lukaku ndie Mchezaji pekee wa Everton aliefunga Bao nyingi, 68.

-Lukaku ni mmoja wa Wachezaji Watatu wa EPL ambao wamemudu kufunga zaidi ya Bao 10 kila Msimu katika Misimu Mitano iliyopita na wengine ni Olivier Giroud na Sergio Aguero.