Thursday, July 13, 2017

RATIBA MPYA LIGI KUU VODACOM 2017/18 YATOKA, KUANZA AGOSTI 26! NGAO YA JAMII YANGA-SIMBA AGOSTI 23, KAGERA SUGAR v MBAO FC

TFF Jana 12/07/2017 ilianika Ratiba Msimu Mpya wa 2017/18 ambao utaanza rasmi kwa Mechi kufungua pazia kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa Yanga na waliobeba FA CUP Simba hapo Agosti 23.
VPL, Ligi Kuu Vodacom, itaanza rasmi Agosti 26 kwa Mechi 7 na Siku inayofuata Mabingwa Yanga kuanza utetezi wa Taji lao Jijini Dar es Salaam kwa kucheza na Timu iliyopanda Daraja Lipuli.
Ule mtanange mahsusi wa Watani wa Jadi, Yanga na Simba, sie tumeubatiza ‘Kariakoo Dabi’ ila wale wanaotukuza mambo wauita ‘Dar Dabi’, utapigwa Oktoba 14, Nyerere Dei, Siku ya kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere.
Simba watafungua Msimu wao wa VPL kwa kucheza Nyumbani na Ruvu Shooting hapo Jumamosi ya Agosti 26.
Michezo mingine ya Siku ya Ufunguzi, Jumamosi ya Agosti 26, itawakutanisha Ndanda wakiwa Wenyeji wa Azam FC wakati Mwadui ikiwakaribisha wapya Singida United, huku Mtibwa ikicheza Nyumbani na Stand United.

Huko Bukoba, Kagera Sugar watakuwa Wenyeji wa Mbao FC na Timu Mpya Njombe Mji ikiwa Nyumbani kuivaa Tanzania Prisons.

Mechi nyingine ya Siku ya Ufunguzi ni huko Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya wakati wa Nyumbani Mbeya City wakikipiga na Majimaji FC.

VPL, LIGI KUU VODACOM
Mechi za Ufunguzi

Jumamosi 26/08/2017

Ndanda v Azam
Mwadui v Singida
Mtibwa v Stand
Simba v Ruvu
Kagera v Mbao
Njombe v Prisons
Mbeya v Majimaji

Jumapili, 27/08/2017
Yanga v Lipuli