Monday, July 10, 2017

UHAMISHO 2017: BEKI ANTONIO RUDIGER ASAINIWA NA CHELSEA

Mabingwa wa England Chelsea wamemsaini Beki wa Timu ya Taifa ya Germany Antonio Rudiger kutoka AS Roma ya Italy kwa Dau la Awali la Pauni Milioni 29.
Rudiger, mwenye Miaka 24, amekamilisha Uhamisho huu ukiwa ni Wiki 1 tu tangu aisaidie Germany kutwaa FIFA Kombe la Mabara kwa kuilaza Chile 1-0 kwenye Fainali.
Chelsea imempa Rudiger Jezi Namba 2 ambayo alikuwa akiivaa Branislav Ivanovic aliehamia Zenit St Petersburg ya Urusi Mwezi Januari.
Kabla ya kujiunga na AS Roma, Rudiger alianza Soka lake Borussia Dortmund kisha kujiunga na Stuttgart Mwaka 2011.

Alijiunga na AS Roma Mwaka 2015 na Msimu wa 2015/16 aliichezea AS Roma Mechi 30 za AS Roma walipomaliza Ligi hiyo Nafasi ya 3 na Msimu wa 2016/17 kucheza Mechi 26 wakati AS Roma ikimaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Juventus.

Rudiger ameichezea Germany Mechi 17.