Thursday, July 6, 2017

UHAMISHO 2017: MAN UNITED YAKUBALI KULIPA £75M KUMNUNUA LUKAKU, LUKAKU KUTUA OLD TRAFFORD KABLA WIKIENDI!

Manchester United wameafiki kulipa Ada inayodaiwa kuwa Pauni Milioni 75 ili kumnunua Straika wa Everton Romelu Lukaku. Kwa kumpata Lukaki sasa inaaminka Man United itaacha kabisa kumfuatilia Straika wa Spain anaechezea Real Madrid Alvaro Morata.
Mpasuko wa Habari hizi Mpya pia umesisitiza kununuliwa kwa Lukaku hakuhusiani na Dili yeyote ya Wayne Rooney kuondoka Man United kwenda Everton.
Uhamisho wa Lukaku kwenda Man United unatarajiwa kukamilika kabla ya Jumapili.