Friday, July 14, 2017

UHAMISHO 2017: MAN UNITED YAMTAKA BEKI WA IVORY COAST SERGE AURIER ANAYAKEKIPIGA PSG

Manchester United wamewasiliana na Paris Saint-Germain kuhusu Beki wao Serge Aurier ahamie Old Trafford kwa mujibu wa chanzo toka Jarida la France Football.
Taarifa hizi zimedai upo uwezekano mkubwa Beki huyo kutoka Ivory Coast mwenye Miaka 24 akawa Mchezaji wa 3 mpya wa Man United baada ya kuwasaini Victor Lindelof na Romelu Lukaku.
Mbali ya kutakiwa na Man United, pia zipo fununu Manchester City, AC Milan, Juventus na Barcelona pia zinamtamani Beki huyo.
PSG wapo tayari kumuuza Aurier kwa kitita cha Pauni Milioni 22 lakini kikwazo kwa Klabu nyingi ni Mshahara wake mkubwa mno.
Aurier, ambae aliichezea PSG Mechi 22 za Ligi 1 Msimu uliopita, amebakiza Miaka Miwili kwenye Mkataba wake na PSG.