Thursday, July 13, 2017

UHAMISHO: IVAN PERISIC AWEKEWA KIZINGITI NA INTER MILAN KWENDA OLD TRAFFORD

Ivan Perisic anataka sana kujiunga na Manchester United lakini Klabu yake Inter Milan inaleta ugumu.
Jana Wakala wa Perisic alikutana na Viongozi wa Inter kujadili Uhamisho huo kwa mujibu wa Sky Sports News HQ.
Tatizo kubwa ni Dau la Uhamisho ambapo Inter wameshikilia walipwe Pauni Milioni 48 kwa Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Croatia.
Man United wametoa Ofa ya Pauni Milioni 39 ambayo Inter wameikataa.
Hivi sasa Perisic yuko kwenye Kikosi cha Inter kilichopiga Kambi ya Mazoezi huko Kaskazini ya Italy na Wiki ijayo kinaruka kwenda Ziarani huko China.
Pande zote mbili, Inter na Man United, wanataka maafikiano yafikiwe kabla Inter kwenda kwenye Tripu yao.
Perisic amekuwa akicheza huko Italy tangu 2015 akipiga Bao 18 katika Mechi 70 za Ligi Serie A baada ya kujiunga na Inter toka Klabu ya Germany Wolfsburg.
Staa huyo mwenye Miaka 28 ameifungia Nchi yake Croatia Bao 16 katika Mechi 57.