Wednesday, July 19, 2017

UHAMISHO: SAMPDORIA YATOA OFA KUMNUNUA JACK WILSHERE

SAMPDORIA ya Italy imetoa Ofa ya Pauni Milioni 6 pamoja na nyongeza kadhaa za Pauni Milioni 1.5 kumnunua Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere.
Wilshere amebakiza Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake na Arsenal na Msimu ulopita alikuwa kwa Mkopo huko Bournemouth.
Hata hivyo Mchezaji huyo mwenye Miaka 25 na ambae ameichezea England mara 34 hakumaliza Msimu baada ya kuvunjika Mguu kwenye Mechi na Tottenham Mwezi Aprili.
Pia iliwahi kuripotiwa kuwa Wilshere atapelekwa kwa Mkopo huko Crystal Palace.
Lakini Wikiendi iliyopita Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alieleza kuwa anatarajia Wilshere atabaki Arsenal na kupigania namba yake.