Monday, July 10, 2017

WAYNE ROONEY HUYOO ARUDI EVERTON

Wayne Rooney, mwenye Miaka 31, ameondoka Manchester United aliyoitumikia Miaka 13 na kurejea Everton alikoanzia Soka lake tangu akiwa Mtoto.
Rooney aliichezea Man United Mechi 559 na kufunga Bao 253 zikiwa ni Bao nyingi kupita Mtu yeyote katika Historia ya Man United.
Akiwa na Man United, Rooney alitwaa Ubingwa wa EPL, Ligi Kuu England, mara 5 na mara moja moja UEFA CHAMPIONS LIGI, UEFA EUROPA LIGI na FA CUP.

Rooney, ambae aliihama Everton Mwaka 2004 kwa Dau la Pauni Milioni 27, sasa amesaini Mkataba wa Miaka Miwili na Everton.