Monday, July 10, 2017

WAZIRI DKT. MWAKYEMBE AWA MGENI RASMI FAINALI ZA SHINDANO LA BONGO STYLE,AKARIBISHA SHINDANO HILO KUFANYIKA BUNGENI DODOMA 2018.


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa hotuba yake wakati wa fainali za shindano la Bongo Style, lililofanyika makumbusho ya Taifa Jijini Dar ,linalohusisha fani za ubunifu wa mavazi,upigaji picha na uandishi wa miswada ya filamu ambapo aliipongeza Taasisi isiyo ya kiserikali ya Faru Arts and Development Organization(FASDO) kwa kuandaa mashindano hayo, alisema kuwa Serikali inalojukumu la kusaidia Asasi kama FASDO ambazo zinaingia katika maswala ambayo Serikali hawakuyawekea msingi mkubwa. "Naomba niagize na kuwa kuna watendaji wetu wa wizara katika sherehe hii mkae chini na watu wa FASDO ili mwaka kesho zoezi hili lifanyikie Bungeni Dodoma" Alisema Dkt. Mwakyembe.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia) akimkabidhi Agnes Nyahonga tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Goodhope Elieskia maarufu kwa jina la Zagamba tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda shindano la Bongo Style katika kipengele cha uandishi wa miswada ya Filamu
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh. Dkt. Harrison Mwakyembe(wa kutoka kulia) akimkabidhi Masoud Masoud tuzo na zawadi ya mfano wa Hundi yenye thamani ya Tsh 1,000,000 aliyeshinda shindano la Bongo Style katika kipengele cha ubunifu wa mavazi.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na MichezoMh. Dkt. Harrison Mwakyembe(wa pili kutoka kulia) akimkabidhi Philip Florian tuzo ya Best Personality aliyopokea kwa niaba ya Kelvin Mwanasoko ambaye hakuweza fika katika Mashindano hayo.