Sunday, July 16, 2017

ZIARA YA MANCHESTER UNITED: LA GALAXY 2 vs MAN UNITED 5, WAPYA LINDELOF NA LUKAKU WACHEZA KWA MARA YA KWANZA

Manchester United new boy Romelu Lukaku failed to score on debut against LA GalaxyMANCHESTER UNITED wameanza Mechi za Ziara yao ya USA kwa kuifunga LA Galaxy 5-2 huko Los Angeles, California ndani ya StubHub Center Mechi ambayo ilichezwa Alfajiri hivi Leo.
Kwenye Mechi hiyo, Man United walifunga Bao lao la kwanza Dakika 2 tu tangu Mechi ianze Mfungaji akiwa Marcus Rashford baada ya mchango wa Jesse Lingard.
Rasford aliongeza Bao la Pili katika Dakika ya 20 na Dakika ya 26 Bao zilikuwa 3-0 Mfungaji akiwa Marouane Fellaini.

United boss Jose Mourinho was pleased with Lukaku's performance despite his lack of goalsKipindi cha Pili kilianza kwa Man United kubadili Timu na kuingiza Kikosi kingine kabisa wakiwemo Wachezaji Wapya Victor Lindelof na Romelu Lukaku.
Man United waliongeza Bao zao 2 kupitia Henrikh Mkhitaryan na Anthony Martial.
LA Galaxy walifunga Bao zao 2 katika Dakika 11 za mwisho kupitia Giovani dos Santos na Dave Romney.

MAGOLI:
LA GALAXY
- Dos Santos 79, Romney 88;
MAN UNITED - Rashford 2, 20, Fellaini 26, Mkhitaryan 67, Martial 72

MAN UNITED - VIKOSI:
Kipindi cha Kwanza:
De Gea, Valencia, Jones, Smalling, Blind, Carrick, Herrera, Fellaini, Lingard, Mata, Rashford.

Kipindi cha Pili: J. Pereira, Tuanzebe, Lindelof, Bailly, Darmian, Fosu-Mensah (Mitchell 85), Pogba, A. Pereira, Mkhitaryan, Martial, Lukaku.
Marcus Rashford ndie aliyeanza kufunga bao
Rashford Antonio Valencia na Marouane Fellainiwakipongezana
Henrikh Mkhitaryan akipongezana na Lukaku


Manchester United – Mechi zao kuelekea Msimu Mpya:
15 Julai v LA Galaxy, Stubhub Centre, Los Angeles [5-2]
17 Julai v Real Salt Lake, Rio Tinto Stadium, Sandy, Utah
20 Julai v Manchester City, NRG Stadium, Houston, Texas (International Champions Cup)
23 Julai v Real Madrid, Levi’s Stadium, Santa Clara, California (International Champions Cup)
26 Julai v Barcelona, FedExField, Washington DC (International Champions Cup)
30 Julai v Valerenga, Ullevaal Stadium, Oslo
2 Agosti v Sampdoria, Aviva Stadium, Dublin
8 Agosti v Real Madrid, National Arena Filip II, FYR Macedonia (UEFA Super Cup)