Saturday, August 19, 2017

EPL FULL TIME : SWANSEA CITY 0-4 MANCHESTER UNITED, POGBA NA LUKAKU WAENDELEZA MAKALI TENA LEO WAKIWATEKETEZA SWANSEA.

Timu ya Manchester United imefunga magoli matatu ndani ya dakika nne na kuendeleza wimbi la ushindi kwa kuibuka na ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Swansea.
Katika mchezo huo Eric Bailly, Romelu Lukaku, Paul Pogba na Anthony Martial walifanikisha kupatikana kwa ushindi huo wa kikosi cha Jose Mourinho.
Jordan Ayew alikuwa wa kwanza kukosa kosa goli kwa kupiga shuti lililogonga mwamba, kabla ya baadaye Eric Bailly kuipatia Manchester United goli la kuongoza.
Romelu Lukaku aliongeza goli la pili kwa Manchester United katika dakika ya 80 kwa shuti la karibu kisha Pogba akafunga la tatu kambla ya Anthony Martial kufunga la nne.
Beki Eric Bailly akiuwahi mpira wa kichwa uliopigwa na Paul Pogba uliogonga mwamba na kuuzamisha kimiyani
Paul Pogba akifunga kiufundi goli la tatu la Manchester United
Anthony Martial akiachia shuti na kufunga goli la nne la Manchester United.

Dakika ya 45 Beki matata Bailly aliwapatia man United bao la kuongoza kipindi cha kwanza. Hadi dakika 45 zinatimia kwenda mapumziko SWANSEA CITY 0-1 MANCHESTER UNITED.
Taswira kabla mtanage kuanza
Meneja wa Swansea Paul Clement akisalimiana na meneja wa Man United  United Jose Mourinho Kipute kikiwa kimeanza.
Martin Olsson akichuana vikali na  Antonio Valencia wa Man united
Jordan Ayew akiachia shuti kaliPhil Jones akiwa ndani ya 18 akiunganisha mpira wa kichwa.


Marcus Rashford na Roque Mesa

Tom Carrollakijiuguza baada ya kufanyiwa rafu na Pogba


Refa Jon Moss akimpa neno Pogba

Pogba
Rashford
Romelu Lukaku Lukaku akithibitisha kwa Mashabiki wapatao 20,862 kuwa yeye ni kiboko.

Henrikh Mkhitaryan akimshuhudia Lukaku akifunga bao.


Pogba akishangilia pamoja na Lukaku baada ya kufanikisha bao 2-0


Pogba nae alipongezwa kwa bao lake
Martial akihangilia bao lake


Martial akishangilia pamoja na wenzake