Thursday, August 17, 2017

JOSE MOURINHO ATAKA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI KABLA YA AGOST 30

London, England. Kocha wa Manchester United anapambana kwa kila namna kuhakikisha dirisha la usajili linapofungwa awe amekamilisha kusajili wachezaji wawili.
Rada za kocha huyo zinaelekea kutua kwa winga Arjen Robben kabla ya kufungwa dirisha la usajili Agosti 31.

Mkataba wa Robben umebaki mwaka mmoja kumalizika kwenye klabu yake ya Bayern Munich na kwa mujibu wa mtandao wa Daily Mail, kuna uwezekano mkubwa wa Mourinho kumnyakua mchezaji huyo wa Bayern Munich.