Saturday, August 12, 2017

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI AGAWA VIFAA VYA MICHEZO JIMBONI KWAKE


MBUNGE wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amegawa vifaa vya michezo kwa timu za jimbo hilo zinazoshiriki mashindano ya kombe la Mazingira linaloshirikisha timu za wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.

Akizungumza na gazeti hili Ridhiwani alisema atawapatia washindi wa pili wa michuano hiyo pikipiki ya miguu miwili na jezi kwa timu zote tatu za juu na mshindi wa kwanza atapata zawadi ya bajaji toka kwa mkuu wa wilaya.
“Tumeamua kutoa zawadi ya pikipiki ili ziwasaidie vijana kuingiza kipato ili kuongeza ajira kwa vijana badala ya kuendelea kuwa tegemezi,” alisema Ridhiwani

Pia Ridhiwani alisema mashindano hayo yameandaliwa na Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bagamoyo kwa kushirikiana na wabunge wa majimbo yote ya wilaya hiyo.
Hafla ya kugawa vifaa ilitanguliwa na mchezo wa soka kati ya timu ya Kata ya Kimange na Mbwewe.