Wednesday, August 23, 2017

MPAMBANAJI, RAHEL PALLANGYO APATA TUZO YA MPIGAPICHA BORA


MPIGAPICHA wa Tanzania Standard Newspapers Ltd na Mmiliki wa mtandao huu Rahel Pallangyo amepata tunzo ya mpigapicha bora wa Mashindano ya Ndondo 2017 yaliyofanyika kwenye      Mkoa wa Dar es Salaam.
Mbali na tunzo hiyo waandaji wa michuano hiyo walitoa tunzo mbalimbali kwa washindi, tunzo binafsi, vikundi na tunzo za heshima.
Tunzo mwamuzi bora ilichukuliwa na Nadim Mohamed, mwandishi bora alikuwa Charles Abel wa Mwananchi, balozi wa Ndondo mchezaji wa Tottenham ya England Victor Wanyama, shabiki bora alichaguliwa Jata Boy wa Misosi FC na Kitoto cha Ndondo.
Kwa upande wa Wachezaji beki bora alikuwa Kashkash Kindamba wa Keko Furniture, kiungo mshambuliaji bora ni Emanuel Pius kutoka timu ya Goms United, mfungaji bora ni Rashid Roshwa wa Kibada One, mchezaji bora akaibuka Emanuel Memba wa Misosi FC.