Sunday, August 20, 2017

QATAR YABAINISHA MPANGO WA UJENZI WA UWANJA WA KISASA KABISA

Mpango wa ujenzi wa uwanja wa sita wa kisasa wenye uwezo wa kuingia mashabiki 40,000 kwa ajili ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2022 Qatar umebainishwa.
Uwanja huo utakaogharimu paundi bilioni 5 uitwao Al Thumama umejengwa katika muonekano wa kofia inayopendwa kuvaliwa na wanaume wa kiarabu 'gahfiya'.

Uwanja wa Al Thumama utakaokuwa na viyoyozi unaojengwa kusini mwa Qatar katika Jiji la Doha ni miongoni mwa viwanja saba vinavyojengwa kwa ajili ya kombe la dunia.
Uwanja utakaotengenezwa kwa muonekano wa kofia unavyoonekana kwa ndani
Uwanja wa Al Thumama utakavyokuwa unaonekana mithili ya kofi