Tuesday, August 29, 2017

TANZANITE KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KAITABA

Timu ya Taifa ya soka ya wasichana waliochini ya miaka 20 ‘Tanzanite’ inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Kaitaba Kagera.
Lucas alisema tarahe ya mchezo huo itatangazwa baada ya timu ambazo zimepelekewa barua ya maombi kuthibitisha na umepelekwa Kagera ili kupunguza gharama kwani inawezekana ikacheza ama na Uganda, Rwanda au Burundi. Tanzanite inatarajia kucheza na Nigeria Septemba 15,16 au 17 kuwania kufuzu fainali za dunia za wanawake.