Thursday, August 31, 2017

FULL TIME: UGANDA 1-0 EGYPT, EMANUEL OKWI AIPIGA MISRI


MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Simba, Emanuel Okwi leo ameisaidia timu yake ya Taifa, “Uganda the Crane’ kuifunga Misri bao 1-0 kwenye mchezo kufuzu fainali za Dunia zitakazofanyika Russia 2018.
Uganda ambayo ilikuwa ikicheza nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa wa Mandela ilipata bao dakika ya 51 likifungwa na Emanuel Okwi kwa shuti baada ya kuichambua ngome ya Misri kutoka upande wa kulia.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Okwi alisema wamefurahi kushinda mchezo huo lakini wanajiandaa kwa mchezo wa marudiano ambao unatarijiwa kuchezwa Alexanderia Misri Septemba 5.

Kocha wa Uganda The Cranes, Moses Basena alisema nilipowaita wachezaji niliwaambia juu ya mchezo huu na ushindi tu lakini kocha wa Misri Hector Cuper alisema uwanja ulikuwa mbaya na walijaribu namna nyingi lakini hawakufanikiwa
“Tuna michezo ya kushinda na tuna pointi 6 hivyo tunaamini tutashinda nyumbani,” alisema Cuper.
Kutokana na mchezo huo wa marudiano Simba itawakosa Okwi na Juuko kwenye mchezo dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Septemba 6.
Kikosi cha Uganda ni Dennis Onyango, Nico Wakiro Wadada, Godfrey ‘Jajja Walu’ Walusimbi, Isaac Isinde, Murushid Jjuuko, Khalid Aucho, Emmanuel Arnold Okwi, Hassan Wasswa Mawanda, Faruku Miya, Derrick Nsibambi, Joseph Benson Ochaya
Kikosi cha Misri ni Essam El Hadry, Fathy, Hegazi, Ramy Rabea, Shafy, Tarek Harmed, Muhammed ElNeny, Hassan ‘Trezegeut’ Mohamoud, Abdalla, Muhamed Salah, Kahraba