Sunday, August 20, 2017

ZLATAN IBRAHIMOVIC YU TAYARI KURUDI UPYA EPL, AKIJIRUSHA MAJINI KUTOKA KWENYE BOTI KUONESHA YUKO FITI

Zlatan Ibrahimovic inaonekana ameanza kupona jeraha lake la goti alilopata baada ya kuonekana akiruka kutoka juu ya boti ya kifahari na kutumbukia majini akiwa Riviera Ufaransa.
Mchezaji huyo raia wa Sweden amekuwa akiharakisha kupona kwake akipitia kipindi cha kuimarisha zaidi mguu ulioumia, na ametumia kipindi hiki kuwa na familia yake huko Cannes.
Zlatan Ibrahimovic akiwa ameruka juu huku familia yake ikimuangalia
Zlatan Ibrahimovic akiwa amechupa kuelekea majini katika kujiweka fiti