Monday, September 18, 2017

GARETH BALE ATUPIA GOLI REAL MADRID IKIIZIMA REAL SOCIEDADBAO 3-1.

Gareth Bale amefunga goli kali wakati Real Madrid ikimaliza rekodi ya ushindi wa asilimia 100 wa Real Sociedad katika msimu huu katika mchezo wa La Liga.
Mchezaji huyo raia wa Wales hakuonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo hadi pale alipofunga goli baada ya kumzidi kasi Kevin Rodrigues.

Mshambuliaji Borja Mayoral aliifungia Real Madrid goli la kwanza tangu ajiunge na klabu hiyo katika mchezo huo uliomalizika kwa ushindi wa magoli 3-1.
Mshambuliaji Gareth Bale akifunga goli la tatu la Real Madrid