Sunday, September 10, 2017

Kiba kuongoza wasanii kibao Tigo Fiesta 2017

Na Mwandishi Wetu, Arusha
TAMASHA kubwa la muziki la Tigo Fiesta 2017 linazinduliwa rasmi leo kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa na kushirikisha wanasanii kibao nyota na chipukizi.
Nyota hao wataongozwa na Ali Kiba (pichani), ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Seduce Me, ambacho kimeipuliwa hivi karibuni na kimepamba vilivyo anga za muziki hapa nchini.

Wapenzi wa muziki watamshuhudia kwa mara ya kwanza Kiba akiimba live kibao hicho, ambacho ni moto wa kuotea mbali.

Baadhi ya wasanii wengine wanaotarajia kufanya vitu vyao katika onesho hilo hilo la leo ni pamoja na Weusi, Darasa, Rostamu, Chege, Dogo Janja, Dogo Aslay, Lulu Diva, Vanessa, Maua, Feza Kessy, Jux, Msaga Sumu, Bright na Jux.

Wasanii wengine ni Ray Vanny, Shishi Baby au Shilole, For Q Ngosha the Don, Madee, Malkia Saida Karoli, Ditto, Christian Bella, Homonize, Foby, Mr Blue na Nandy.

Baadaya Arusha, msimu wa Tigo Fiesta utaelekea Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora, Dodoma, Iringa, Songea, Njombe, Sumbawanga,Morogoro, Tabora na mwisho litatua jijini Dar es Salaam Novemba 11