Monday, September 18, 2017

MANCHESTER UNITED YAIFANYIA KITU MBAYA EVERTON OLD TRAFFORD, YAINYUKA BAO 4-0

Mshambuliaji Romelu Lukaku amefunga goli dhidi ya timu yake ya zamani na kutengeneza moja lingine wakati Manchester United ikiifunga Everton magoli 4-0.
Mchezo huo ulishuhudia Kapteni wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney akirejea Old Trafford kwa mara ya kwanza akiwa na Everton.
Katika mchezo huo Manchester United ilipata goli la kwanza kupitia kwa Antonio Valencia, kisha Henrikh Mkhitaryan akafunga la pili, Lukaku la tatu na Anthony Martial la nne.
Henrikh Mkhitaryan akiifungia Manchester United goli la pili baada ya kupigiwa pande na Romelu Lukaku
Anthony Martial akiifungia Manchester United goli la nne kwa mkwaju wa penati