Friday, September 22, 2017

MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED NA LIVERPOOL WAPEWA ONYO KALI MOSCOW

Related imageMashabiki wa Liverpool na Manchester United wameambiwa kwamba kutakuwa na maafisa wengi wa polisi mjini Moscow wiki ijayo.
Klabu hizo za premia zote zina mechi za klabu bingwa Ulaya katika mji mkuu wa Urusi.

Takriban mashabiki 2,000 watasafiri kuelekea kaskasini magharibi ambapo Liverpool itacheza dhidi ya Spartac Moscow siku ya Jumanne na United ikikabiliana na CSKA Moscow siku ya Jumatano.

Manchester United's Europa League clash against Liverpool at Old Trafford ended in crowd trouble after a Liverpool flag was unfurledUnited imewaambia mashabiki wake kutovaa rangi za klabu hiyo ama hata kutembea Moscow wakiwa peke yao.

Liverpool inasema kuwa mamlaka ya Urusi inajua kwamba vilabu hivyo viwili viko mjini Moscow wakati mmoja kwa hivyo maafisa wengi wa polisi wanatarajiwa mahali popote ambapo mashabiki wa Liverpool na Manchester United watakongamana. Ikiwemo katika maeneo ya malazi.

Mashabiki sugu wa Urusi waliwashambulia wenzao wa Uingereza mjini Marseille katika kombe la bara Ulaya 2016.

TAZAMA PICHA ZAIDI