Friday, September 15, 2017

MBEYA CITY YAMTUPIA VIRAGO KOCHA PHIRI


By MWANAHIBA RICHARD

SAA chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, kuingilia kati ishu ya mishahara ya kocha, Kinnah Phiri uongozi wa Mbeya City umeamua kuvunja mkataba na kocha huyo Mmalawi.

Makalla aliamua kuingia katibaada ya kusikia Mmalawi huyo amepiga hodi ofisi za Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) kulalamika.
Awali TFF ilimwahidi Phiri kumlipa fedha hizo Dola 15,000 (zaidi ya Sh30 milioni) mbali na mkataba wake ambao unadaiwa kutaka kuvunjwa na umebakiza miezi 18.

Phiri alisema juzi Jumanne alionana na RC huyo na kuzungumza naye juu ya mkataba wake na madai anayowadai Mbeya City na baada ya kikao hicho, Makalla aliamuru kuitishwa kikao cha Bodi ya Wakurugenzi ili kujadili na kumpa ripoti ya hatma yake.

Lakini jana jioni unozi wa Ciy ulithibitsha kuvunja mkata na koha huyo baada ya kuafikiana.

Katibu Mkuu wa City, Emmanuel Kimbe alisema; “Tumeafikiana kuvunja mkataba na Kocha Phiri na tutamlipa miezi mitatu ndani siku mbili zijazo.”
Hata hivyo kocha alikiri suala, lakini alisisitiza kuwa, makubaliano yao ni kamna mkataba utavunjwa mara atakapolipwa stahiki yake ya mshahara, huku akimshukuru Mkuu wa Mkoa, aliyeda alipigiwa simu na Rais wa TFF kumweleza tatizo.