Monday, September 18, 2017

PAMBANO LA GENNADY GOLOVKIN NA SAUL 'CANELO' ALVAREZ LAISHIA KWA SARE TATA

Pambano la dunia la uzito wa kati la Gennady Golovkin dhidi ya bondia Saul 'Canelo' Alvarez limemalizika kwa sare yenye utata.
Baada ya kupambana mabondia hao Jijini Las Vegas Jaji wa kwanza alitoa alama 118-110 kwa Alvarez, wa pili alama 115-113 kwa Golovkin na wa tatu sare ya alama 114-114.

Mashabiki walizomea baada ya kutolewa uamuzi huo na majaji katika ukumbi wa T-Mobile Arena, na mabondia wote wawili walitikisa vichwa vyao kuonyesha kutuafiki.

Kwa matokeo hayo Kazakh Golovkin, 35, amebakia na mikanda yake ya WBA, WBC na IBF na kuendelea kuwa na rekodi ya kutopigwa katika mapambano 38.

Bondia Gennady Golovkin akiwa amempiga ngumi ya kushoto Saul 'Canelo' Alvarez
Ngumi ya kulia ya Saul 'Canelo' Alverez ikimpata kidevuni bondia Gennady Golovkin
Mabondia wote wakishangilia na makocha wao baada ya pambano hilo kumalizika bila KO