Friday, September 8, 2017

PEP GUARDIOLA ASEMA HANGEWAPA ARSENAL RAHEEM STERLING

Meneja wa Manchester Pep Guardiola amesema hakukuwa na uwezekano wowote kwamba Manchester City wangemuongeza Raheem Sterling kwenye mkataba wa kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez.
Arsenal walikuwa wameafikiana na City uhamisho wa £60m kwa Sanchez, 28, lakini hilo lilitegemea kufanikiwa kwa Gunners kumchukua Thomas Lemar.
Lemar hata hivyo aliamua kusalia Monaco.
Guardiola amesema Gunners walitaka Sterling, 22, kama sehemu ya mkataba wa kumuuza Sanchez.
"Walizungumza nami. Lakini nikasema haiwezekani," amesema Guardiola.
"Tulisema tulitaka kuwalipa pesa taslimu kwa ajili ya Alexis. Walikubali lakini hawangeweza kumnunua mchezaji waliyemtaka, kwa hivyo alisalia Arsenal."

Sterling amechezea City mechi tatu msimu huu na kufunga mabao mawili.
Image result for raheem sterlingAlifukuzwa uwanjani kwa kusherehekea sana bao la dakika za mwisho la ushindi dhidi ya Bournemouth kabla ya mapumziko ya kimataifa.

Alichezea England mechi mbili wakati wa mapumziko ya kimataifa.