Monday, September 18, 2017

PETR CECH ACHANGIA KUINYIMA USHINDI CHELSEA STAMFORD BRIDGE, DAVID LUIZ AONESHWA KADI NYEKUNDU

Kipa wa zamani wa Chelsea, Petr Cech, amechangia kwa kiasi kikubwa kuinyima ushindi timu hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza ulioishia kwa sare tasa dhidi ya Arsenal katika dimba la Stamford Bridge.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kikosi chake kilibadilika mno baada ya kuchakazwa na Liverpool katika mchezo uliopita na kuambulia pointi ya kwanza nyumbani kwa Chelsea baada ya miaka sita.

Katika mchezo huo beki wa Chelsea, David Luiz alijikuta akipata kadi nyekundu kwa kumchezea rafu ya kizembe mchezaji Sead Kolasinac, na refa Michael Oliver kumtoa nje kwa kadi.
Beki Mbrazil David Luiz akicheka baada ya refa kumpatia kadi nyekundu kwa kucheza rafu
Kocha wa Chelsea Antonio Conte akionekana kukerwa na maamuzi ya refa Michael Oliver