Sunday, September 10, 2017

VPL: KAGERA SUGAR 1 vs 1 RUVU SHOOTING, VENANCE LUDOVIC AOKOA JAHAZI KAITABA LEO.

Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza leo dhidi ya Timu ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo hii kwenye Mchezo  wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.
Kikosi cha Timu ya Ruvu Shooting kilichoanza leo dhidi ya Timu ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo hii kwenye Mchezo wa pili wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.
Picha ya Pamoja

Na Faustine Ruta, Bukoba
Timu ya soka ya Kagera sugar imelazimisha sare ya kufungana bao 1 kwa 1 na timu ya soka ya Ruvu shooting katika mzunguko wa Ligi kuu Vodacom Tanzania bara ikiwa ni mzunguko wa kwanza tangu ligi imeanza mwezi uliopita mchezo ambao umepigwa katika uwanja wa nyumbani wa Kaitaba Bukoba Mjini.

Ligi kuu Vodacom Tanzania bara timu ya kagera sugar kwa mara ya kwanza katika mzunguko huo ulioanza August 26 kagera sugar ilifungwa na Mbao Fc ya Jijini Mwanza bao 1 kwa 0 huku Ruvu shooting  ikifungua Dimba vibaya kwa kupigwa na timu ya Simba Sc bao 7 kwa 0 ambapo timu zote mpaka sasa  zina Alama sawa ya  moja moja.

Katika mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Shomari Lawi ulianza kwa saa kumi za jioni huku wachezaji wa kagera sugar wakianza mchezo huo wakiwa wamepoa na timu ya ruvu shutingi wakianza kwa mashambulizi makali dhidi ya Kagera Sugar

Ruvu shooting walikuwa wa kwanza kwa kufungua lango la timu ya kagera sugar kwa kujipatia goli la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wa timu hiyo Ishara Juma dakika 16.

Licha ya timu ya Ruvu shooting kuwa wa kwanza kupata bao 1 kipindi cha kwanza pia ilikuwa ya kwanza mchezaji wake namba 13 George Wawa kupewa kadi nyekundu muda mfupi baada ya kumfanyia rafu mbaya Mchezaji wa Kagera Sugar V. Ludovick aliyeingia kipindi cha pili cha mchezo huo. 

Dakika ya 75 kagera sugar wamepata fursa ya kusawazisha kupitia kwa mchezaji huyo huyo  Venance Ludovick na mtanange kumalizika kwa kwa sare ya bao 1-1. Wachezaji wa Ruvu Shooting wakifurahia ushindi wa bao lao kipindi cha kwanza lililofungwa na Ishara Juma dakika katika dakika ya 16.
Kipindi cha pili Kagera Sugar waliliandama mara kwa mara Lango la Timu ya Ruvu Shooting na huku Ruvu wakiwa pungufu 10 uwanjani.

Patashika kwenye lango la Timu ya Ruvu Shooting
1-1 Ludovick akishangilia bao lake
Shangwe! 1-1
Baadhi ya Wachezaji wa Kagera Sugar wakimpongeza Ludovick(kulia) kipindi cha pili baada ya kufanya 1-1.

Mchezaji wa Kagera Sugar aliyesajiliwa msimu huu Venance Ludovick ambaye ameisawazshia bao leo hii Kagera. Timu ya Kagera Sugar sasa itaelekea Mjini Dar es Salaam kucheza na Timu ya Azam Fc kwenye Uwanja Chamazi.