Tuesday, October 24, 2017

EDINSON CAVANI AIOKOA PSG KWA KUUMALIZA SARE, NEYMAR AKITOLEWA NJE KWA KADI NYEKUNDU


Edinson Cavani amefunga goli kali la mpira wa adhabu katika dakika ya 93 na kuiokoa Paris St-Germain kuambulia sare ya magoli 2-2 dhidi ya Marseille baada ya Neymar kutolewa nje.
Luiz Gustavo alifunga goli la kwanza la Marseille kwa shuti la umbali wa yadi 30, kabla ya Neymar kusawazisha likiwa ni goli lake la kumi tangu atue PSG.

Florian Thauvin aliifanya Marseille iongoze tena zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya Neymar kupewa kadi za njano mara mbili ndani ya dakika mbili.


Mbrazil Neymar akiwa haamini baada ya kulambwa kadi nyekundu

Mpira uliopigwa na Edinson Cavani ukijaa wavuni na kuiokoa PSG kutoka sare