Sunday, October 1, 2017

EPL: MANCHESTER UNITED YAIBAMIZA CRYSTAL PALACE 4-0

The former Everton star is mobbed by his Manchester United team-mates including a delighted LukakuKlabu ya Manchester United imeonyesha mchezo mzuri na kuweza kuicharaza Crystal Palace 4-0 na hivyobasi kuilazimu klabu hiyo kupoteza mechi yake ya saba msimu huu bila kufunga bao.
Fellaini, the former Toffees midfielder, points to Young to thank him for his assist after grabbing his side's second goalUnited ambao hawajapoteza waliongoza baada ya dakika tatu wakati Marcus Rashford alipowachanganya mabeki wa Palace na kutoa pasi nzuri kwa Juan Mata aliyecheka na wavu akiwa umbali wa maguu 10.
Bao la pili lilijiri baada ya Ashley Young kupiga krosi ambayo ilifungwa na Marouane Fellaini.
Fellaini alifunga bao la pili kupitia kichwa cha karibu kufuatia mkwaju wa adhabu uliopigwa na Rashford mapema katika kipindi cha pili.
Romelu Lukaku alifunga bao la nne kunako dakika za lala salama likiwa bao la 11 katika mechi 10 za United, kwa kumaliza krosi iliopigwa na Martial.
Matokeo hayo yanaipeleka United katika kilele cha jedwali kwa muda mchache huku Manchester United ikialikwa na Chelsea huko darajani.


Crystal Palace wakiwa hoi baada ya kushindwa kufunga hata bao moja kwenye mchezo huo
Juan Mata Mata akimfunga kipa wa Crystal Palace
Marcus Rashfordakifurahia ushindi na Mata
Mata, akipeta vilivyo baada ya kufunga bao.