Sunday, October 22, 2017

FULL TIME: CHELSEA 4 vs 2 WATFFORD

Chelsea imeonyesha uwezo wa kupigana hadi dakika za mwisho na kuibuka na ushindi baada ya kufunga magoli mawili ya dakika za mwisho, ikitokea nyuma na kuibuka na ushindi wa magoli 4-2 dhidi ya Watfford.
Katitika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge, alikuwa Pedro aliyoipatia Chelsea goli katika dakika ya 12, kabla ya baadaye beki ya Chelsea kuzembe na kuruhusu magoli mawili.
Michy Batshuayi aliifungia Chelsea goli la kusawazisha kabla ya baadaye Cesar Azpilicueta kufunga goli la tatu katika dakika ya 87 kabla ya Batshuayi kuongeza goli lake la pili na kufanya matokeo kuwa 4-2.
Michy Batshuayi akiupiga kwa kichwa mpira uliozaa goli la pili la Chelsea
Cesar Azpilicueta akiifungia Chelsea goli la tatu kwa mpira wa kichwa