Tuesday, October 24, 2017

LA LIGA: REAL MADRID YAREJEA KATIKA NAFASI YA TATU BAADA YA KUICHAPA 3-0 EIBAR


Timu ya Real Madrid imerejea katika nafasi ya tatu ya msimamo wa La Liga, baada ya kupata ushindi wa kiulaini wa magoli 3-0 dhidi ya timu ya Eibar iyoyosuasua.
Mabingwa hao watetezi waliongoza kwa magoli 2-0 hadi kipindi cha pili, yaliyopachikwa na Paulo Oliveira aliyejifunga na kisha Isco kutumbukiza la pili.
Cristiano Ronaldo hakufanikiwa kutikisa nyavu, lakini alikuwa beki Marcelo aliyetikisa nyavu na kufunga goli la tatu baada ya kugongeana vyema na Karim Benzema.


Mchezaji wa Eibar Paulo Oliveira akijifunga wakati akijaribu kuokoa mpira

Beki wa Eibar, Arbilla akimkata kwanja beki wa Real Madrid Mfaransa Theo Hernandez