Sunday, October 22, 2017

MANCHESTER CITY YAJICHIMBIA ZAIDI KILELENI LIGI KUU YA UINGEREZA KWA KUICHAPA 3-0 BURNLEY

Sergio Aguero ameifikia rekodi ya mfungaji aliyeifungia Manchester City magoli mengi wakati Manchester City ikiifunga Burnley magoli 3-0 na kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano.
Goli la Aguero la kipindi cha kwanza alilofunga kwa penati iliyotolewa kwa utata limemfanya afikishe magoli 177 kuifungia klabu hiyo sawa na mchezaji wa zamani wa Manchester City Eric Brook.
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola alimkumbatia kwa furaha Aguero wakati mchezaji huyo wa Argentina alipotoka uwanjani huku mashabiki wakisimama jukwaani kuonyesha heshima kwake.
Sergio Aguero akifunga kwa kutulia mpira wa penati iliyotolewa kwa utata
Beki Nicolas Otamendi akifunga kwa kichwa mpira wa kona iliyopingwa na Kevin De Bruyne