Wednesday, October 25, 2017

MANCHESTER UNITED YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA CARABAO KWA KUICHAPA KIULAINI BAO 2-0 SWANSEA CITY


Mabingwa watetezi wa kombe la Carabao Manchester United wametinga robo fainali ya michuano hiyo kiulaini kwa kupata ushindi mwepesi wa magoli 2-0 dhidi ya Swansea City. Kikosi cha Manchester United kilichofanyiwa mabadiliko makubwa kiliutawala mchezo huo na kupata goli la kwanza kupitia kwa Jesse Lingard kufuatia pande la kisigino la Marcus Rashford.

Wageni Manchester United waliongeza goli la pili kwa shambulizi zuri ambapo mpira ulimkuta Lingard na kufunga kwa mpira wa kichwa.


Jesse Lingard akipiga mpira uliozaa goli la kwanza la Manchester United

Mshambuliaji Marcus Rashford akiwatoka wachezaji wa Swansea City