Sunday, October 22, 2017

MIAKA 20 YA MALTCHOICE YAWAKUSANYA MASTAA KIBAO, DAR ES SALAAM

SERIKALI imeitaka Kampuni ya Maltchoice Tanzania kupunguza bei ya kulipia king’amuzi kwa mwezi ili iwe rafiki kwa wateja na kuongeza watumiaji.
Hayo yalisemwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu katika sherehe ya kutimiza miaka 20 ya kutoa huduma nchini Tanzania iliyofanyika Dar es Salaam.
“Niwapongeze kwa kufikisha mihongo miwili ya kutoa huduma, mimi ni mtumiaji wa king’amuzi chenu na napenda kuangalia vipindi vya Eva na Maisha Magic Bongo kwani inasaidia kupumzisha akili baada ya kuchoka,” alisema