Sunday, October 1, 2017

MTIBWA SUGAR YAZIDI KUKAA KILELENI BAADA YA SULUHU NA YANGA.


Beki wa Yanga akiwania mpira na beki wa Mtibwa, Stahimili Mbonde (kulia) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanznaia Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam leo na kumalizika kwa suluhu.

Mashabiki hawaamini kuwa dakika 90 zimeisha kwa suluhu

Daktari Bavu akimwangalia Ngoma
YANGA imeshindwa kutumia vema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa suluhu na Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
Hii ni sare ya tatu kwa Yanga tangu kuanza msimu huu baada ya kutoka suluhu na Lipuli kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na Majimaji na kwa Mtibwa ni ya pili.
Matokeo hayo yanaifanya timu hiyo ishike nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi tisa.
Katika mchezo huo timu zote zilishambuliana kwa zamu, wenyeji Yanga wakitawala kipindi cha kwanza na wageni kipindi cha pili.
Yanga ilianza kukosa mabao kuanzia dakika ya 26 ambapo Ibrahim Ajib alipiga shuti kali lililopanguliwa na kipa wa Mtibwa Sugar, Benedict Tinoco.
Yanga ilikosa bao lingine katika dakika ya 52 ambapo mchezaji wake, Raphael Daudi shuti lake lilipanguliwa na kipa wa Mtibwa, Tinoco.
Aidha Mtibwa ilikosa bao katika dakika ya 60 ambapo shuti la Salum Kihimbwa lilipanguliwa na kipa wa Yanga, Youthe Rostand.
Kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma, wenyeji Singida United wamepunguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Azam.
Matokeo hayo yanaifanya Mtibwa na Azam kuendelea kulingana pointi baada ya zote kuwa na pointi11, Mtibwa ikiongoza kwa uwiano mzuri wa mabao.
Huko Mwanza wenyeji Mbao walilazimishwa sare ya bao 1-1 na Prisons, wenyeji wakichomoa bao hilo dakika za mwisho.
Bao la wageni Prisons lilifungwa na Eliuter Mpepo katika dakika ya 48 na lile la Mbao likifungwa na Rajesh Kotecha dakika ya 84.
Aidha mechi nyingine zilizochezwa Mwadui ililazimishwa sare ya mabao 2-2 nyumbani dhidi ya Mbeya City, Majimaji ikitoka suluhu nyumbani dhidi ya Kagera Sugar na Ruvu Shooting ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na Njombe Mji.