Saturday, October 28, 2017

SANGA ATEUA WAJUMBE 12 KAMATI YA LIGI

MWENYEKITI wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga ameteua wajumbe 12 akiwemo yeye mwenyewe watakaounda kamati ya bodi ya ligi katika kikao kilichofanyika juzi.
Katika taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari na Boniface Wambura ambaye ndiye Katibu wa kamati hiyo inasema kamati itashughulikia uendeshaji na usimamizi wa Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili
“Kamati itaongozwa na Mwenyekiti mwenyewe, Shani Mligo ambaye ni Makamu Mwenyekiti, Boniface Wambura ambaye ni Katibu, wajumbe ni Issa Batenga, Leslie Liunda na Wakili Saleh Njaa,” alisema Wambura.
Wengine ni Dk. Ellyson Maeja, George Malawa, Isaac Chanji, Baruan Muhuza, Mbakileki Mutahaba na Ally Mayay.
Pia Sanga amewateua Kanali Charles Mbuge ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Ruvu Shooting, na Abuu Changawa (Majeki) kuingia kwenye kamati ya uongozi ya TPLB kwa mujibu wa Ibara ya 28(vi) ya Kanuni za Uendeshaji za TPLB ambayo inampa nafasi ya kuteua wajumbe wawili