Thursday, November 2, 2017

BEKI PSG ATUPIA HAT-TRICK NA KUCHANGIA USHINDI WA KIPIGO CHA MKONO 5-0


Beki wa kushoto Layvin Kurzawa amekuwa beki wa kwanza kufunga magoli matatu yaani hat-trick wakati Paris St-Germain ikiichakaza Anderlecht kwa magoli 5-0 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Beki Kurzawa alikuwa amefunga magoli 17 tu kabla ya kuanza kwa mchezo huo wa jana usiku alifanikiwa kupachika magoli hayo matatu katika kipindi cha pili.

Mbrazil Neymar na Marco Verratti nao pia walifunga magoli mawili mazuri na kuifanya PSG na kufuzu hatua ya mtoano.


Marco Verratti akiwa ameachia shuti lililozaa goli

Beki Layvin Kurzawa akiwa amefunga goli lake la pili kati ya matatu