Thursday, November 2, 2017

CHELSEA YAWA TIMU YA KWANZA UINGEREZA KUFUNGWA UEFA MSIMU HUU, 3-0 NA ROMA


Chelsea imekuwa timu ya kwanza ya Uingereza kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya katika msimu huu baada ya kufungwa magoli 3-0 na wenyeji Roma.
Roma walipata goli la kwanza kupitia kwa Stephan El Shaarawy, kwa shuti la umbali wa yadi 25, kisha baadaye Alvaro Morata akakosa nafasi ya kusawazisha.

El Shaarawy tena akafunga goli la pili baada ya beki Antonio Rudiger kushindwa kuudhibiti mpira uliopigwa na Radja Nainggolan, kisha Diego Perotti akafunga goli la tatu.


Stephan El Shaarawy akifunga goli la kwanza la Roma

Diego Perotti akiwa ameachia shuti lililozaa goli la tatu