Thursday, November 2, 2017

ERASTO NYONI MCHEZAJI BORA WA SIMBA OKTOBA

Image result for erasto nyoni
MCHEZAJI Kiraka wa Simba Erasto Nyoni ameibuka mchezaji bora wa klabu hiyo kwa mwezi Oktoba baada ya kuonesha kiwango cha juu katika mechi nne na kuzawadiwa sh 500,000.
Erasto ambaye anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani amekuwa chachu ya matokeo mazuri kwa Simba tangu asajiliwe akitokea Azam FC msimu huu.
Katika taarifa iliyotolewa na SimbaApp inasema katika mwezi Oktoba Simba ilicheza mechi nne na Erasto alicheza vizuri na kuisadiwa timu kupata matokeo mazuri.
“Katika mechi dhidi ya Njombe alichangia upatikanaji wa jumla ya mabao matatu katika mechi hizo nne tangu ligi ianze akiwa ametoa pasi sita za mabao na yeye akifunga moja,” ilisema taarifa hiyo.
Mechi ambazo Erasto alisaidia timu yake ni dhidi ya Stand United, Mtibwa Sugar, Njombe Mji na Yanga ambapo walishinda mechi mbili na kutoka sare mbili.
Kuanzia ligi inaze msimu huu tuzo ya mchezaji bora Agosti ilikwenda kwa mshambuliaji Emanuel Okwi na Septemba ilichukuliwa na kiungo mshambuliaji Mzamiru Yassin.

Simba imeondoka leo kwa ndege kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bbara dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa Jumapili katika Uwanja wa Sokoine.