Thursday, November 2, 2017

LIVERPOOL YAKARIBIA KUTINGA HATUA YA MTOANO YA LIGI YA MABINGWA ULAYA , YAFUNGA BAO 3-0


Timu ya Liverpool imekaribia kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2008-09 kwa kupambana mno na kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Maribor.
Mshambuliaji Mohamed Salah alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu kwa kufunga kifundi, huku baadaye James Milner akishuhudia penati yake ikiokolewa na kipa Jasmin Handanovic mwenye miaka 39.
Kiungo Emre Can aligongeana vyema na Milner na kisha kuachia shuti la mpira wa kuzungusha uliomkuta Daniel Sturridge aliyefunga goli la tatu.


Mohamed Salah akifunga goli la kwanza la Liverpool
Mshambuliaji Daniel Sturridge akifunga goli la tatu la Liverpool