Thursday, November 2, 2017

SERGIO AGUERO AWEKA REKODI WAKATI MAN CITY IKISHINDA 4-2


Mshambuliaji Sergio Aguero amekuwa mfungaji aliyeifungia Manchester City magoli mengi katika kipindi chote wakati wakiifunga Napoli kwa magoli 4-2 na kutinga hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mchezo huo Manchester City ilitokea nyuma na kuibuka na ushindi na kuifunga Napoli ambayo haijafungwa hadi sasa katika ligi ya Serie A. Lorenzo Insigne aliifungia Napoli goli la kwanza.
Nicolas Otamendi akafunga goli la kusawazisha Jone Stones kaongeza goli la pili, Frello Fillo akaifungia Napoli goli la pili, kisha Sergio Aguero akaifungia Manchester City goli la tatu na baadaye Raheem Starling.


Kipa wa Napoli akiruka bila ya mafanikio mpira uliopigwa na Jone Stones

Mshambuliaji Sergio Aguero akiachia shuti na kufunga goli la tatu la Man City